GET /api/v0.1/hansard/entries/1547402/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547402,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547402/?format=api",
"text_counter": 935,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": "Ifahamike kuwa, magaidi ama wezi wa mifugo sio jamii kwa ujumla, bali ni mtu mmoja katika hiyo jamii – it is an individual . Hawasimamii jamii nzima. Usije ukadanganyika kuwa jamii fulani ni ya magaidi. Ni wananchi wachache ambao wanajulikana. Ombi langu ni kuwa, Serikali iweze kufanya proper disarmament . Janga hili la magaidi limeiletea Serikali hasara. Ninaongea kuhusu Kerio Valley upande wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Jumamosi, nilikuwa katika Kata ya Chesumen, Kerio Valley, Aror. Pia, nilienda Tunyo, Chepkum, Aror kwenyewe na Niwai katika Kata ya Aror. Katika maeneo hayo yote, wananchi wanaomba wizi wa mifugo ufike kikomo. Kule, kuna ardhi nzuri iliyo na rotuba nyingi, na inaweza kulisha Kenya nzima. Tutafanyaje hayo yote tukiwa na terrorists ama bandits ? Itabidi tubadilishe sheria ili yeyote atakayepatikana katika Bonde la Kerio…"
}