GET /api/v0.1/hansard/entries/1547406/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547406,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547406/?format=api",
"text_counter": 939,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": " Magaidi hao wamefanya watu wahame kwao. Pia, wamefanya vijana wadogo wasalie nyumbani badala ya kutafuta riziki ama kutafutia jamii zao maisha bora huko Eldoret na miji mingine kama wenzao. Hii ni kwa sababu hawawezi kuwaacha mama na jamii zao bila ulinzi. Nikipigiwa simu na mtu yeyote kutoka Bonde la Kerio, haswa kabla haijatimia saa sita mchana, huwa ninashikwa na hofu moyoni mwangu na kushangaa iwapo ni uvamizi umefanyika ama ni jambo lipi limetokea. Ninashukuru Kamati hii ambayo mimi pia ni mwanachama. Nilitembea katika hizo Kaunti zote. Ninazidi kusisitiza Serikali ikaze kamba kwa sababu tunapoteza rasilimali nyingi. Watu hao wanaeza kujiendeleza, kupanda vyakula na kuilisha Kenya nzima."
}