GET /api/v0.1/hansard/entries/1547579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1547579,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547579/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ni ya kulaghaiwa kwa vijana wetu ambao wanatafuta ruzuku kule ughaibuni. Ni muda mrefu tumekuwa tukifuatilia katika kamati yetu leba vile vijana wamekuwa wakinyang’anywa pesa zao, wakiuza mashamba wakidanganywa kwamba wataenda kupata masomo ama kupata kazi huko nje. Inasikitisha kuwa ni wizara ya serikali, inayoongozwa na Waziri. Zinatangazwa fursa, waziri anakwenda pale, watoto wanapewa offer letters, wananyang’anywa tu kima cha Shilingi 50,000 na zaidi. Tuko na ushaidi wa kutosha. Kauli yangu ni kusema nalaani na kukashifu vikali kitendo kama hicho. Haiwezekani kwamba tunasema tunajaribu kunyorosha maajenti ambao wamekuwa wakiwaibia watoto wetu. Sasa imekuwa ni ma boardroom ya waziri ambayo yanatumika watoto hawa kulaghaiwa. Hii haingekuwa Statement, Sen. Gloria. Ungemuacha Waziri aje hapa ajibu Maseneta wote 67 wa taifa la Kenya. Atuambie vile anatuambia kuwa anasafisha maajenti wezi alafu inageuka hata zile fursa ambazo Rais ameenda kutuombea kule nje, anaanza kuibia vijana wetu hapa. Asante, Bw. Spika."
}