GET /api/v0.1/hansard/entries/1547628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1547628,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547628/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Mstahiki Spika, kwa kunipa nafasi kuchangia na kutoa tafsida yangu kwa Taarifa iliyoletwa na Sen. Orwoba. Wakati huu nchi inapambana kuhakikisha kwamba vijana na wananchi kwa jumla wanapata kazi hapa na nchi za nje. Ni jambo la aibu kuona watu wakiritimba wamejipanga kuhadaa Wakenya. Hakuna jambo mbaya kama mawakala tisa wameungana na benki tatu kuhakikisha kwamba wamewalaghai wanaotafuta kazi. Waziri wa Leba na Maslahi ya Jamii anafaa kujua mambo haya yote kabla hayajafika hapa. Kama amemakinika anafaa kujua kuna jambo linaendelea kule nje na Wakenya wanapoteza fedha zao. Bwana Spika, mambo ni wawili- iwe anafahamu kinachoendelea au la. Kama hajui, tuko hapa kumkumbusha ya kwamba yanayotendeka ni aibu. Wakati Waziri atakapokuja hapa, atakuja kulia na sisi. Machozi ya mtengeneza jeneza hayafai kuchukuliwa kwa uzito katika mazishi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}