GET /api/v0.1/hansard/entries/1547629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547629,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547629/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Tunao ushahidi ni akina nani wanafanya mambo hayo. Tunajua inaendelezwa katika ofisi zipi. Wanaotenda hayo wanafanya sinema ya Kichina kutuonyesha wanavyopeleka watu nchi za nje. Watoto wetu bado wako kule mashinani na pesa zao zimepotea. Benki inaitisha Shilingi 5,000 kutoa mkopo ili ilipe moja kwa moja kwa wale mawakala bila kupitia kwa wale wanaotafuta kazi. Imefika wakati ambao sisi kama Seneti tunafaa kusimama tusichukuliwe kama wanasesere kwa sababu tunajua tunayofanya."
}