GET /api/v0.1/hansard/entries/1547961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1547961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1547961/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Swali langu linahusu muda. Bw. Waziri, waswahili husema, mnyonge mnyongeni na haki yake mpe. Umesema ya kwamba kuna mazungumzo ambayo yanaendelea ili kuhakikisha kwamba wale ambao hawakulipwa pesa zao waweze kuzipata. Ukipiga hesabu, utapata ya kwamba takriban miaka 27 zimeisha. Wengi wao walikufa wakingojea pesa zao. Bw. Waziri, ingekuwa wewe, ungeweza kungoja pesa kwa miaka karibu 30 ilhali uko na matumizi ya hizo pesa? Je, inawezekana utupe muda ambao unaona kama unakadiria? Hili jambo linaweza kumaliziwa ili hawa watu waweze kufaidika na pia waweze kupata nafuu kwa sababu pesa zao zimekaa kwa muda mrefu sana. Nchi hii inashikiliwa sana na wakulima. Vyama nyingi vya ushirika ambavyo vimeanguka huwa zinaenda na pesa za wakulima. Hii hutendeka kwa sababu ya uongozi mbaya katika vyama vya ushirika. Unafanya nini kuhakikisha ya kwamba jambo ambalo lilifanyika katika KCC halitarudiwa tena?"
}