GET /api/v0.1/hansard/entries/1548015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1548015,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1548015/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Mstahiki Spika. Kwanza nikushukuru kwa swali ambalo umeuliza kuhusu vyama vya ushirika kufilisika. Jambo la kwanza, sababu kubwa huwa uongozi mbaya kwa vyama vya ushirika na wale wanaoongoza vyama vile kule mashinani. Bw. Waziri, unajua tukianza kutatua tatizo, lazima tuweke msingi. Kulikuwa na sababu kubwa ambayo ilifanya Kimuri kufilisika. Inafaa kuangaliwa kwa kina ilifisika kwa nini. Tunapojaribu kuongeza kuzalisha kahawa, na wakulima bado wanaenda kilomita 10 kupeleka kahawa kwa mitambo ya kusagia, wengi wataenda kulima vitu mimmea nyingine ambayo haina maana kushinda kahawa. Kitu ambacho ningeambia Bw. Waziri ni kwamba chanzo kubwa ya kufilisika kwa vyama vya ushirika ni maafisa ambao wako katika Wizara yake. Nasema hivyo kwa sababu juzi, mwaka uliyopita, kule Kirinyaga, Kibirigwi na Mutira farmers cooperatives, karibu zifilisike kwa sababu ya mikopo iliyochukuliwa na maafisa kutoka Wizara yako. Walikopa pesa watu binafsi halafu wakakata wakulima. Ni jambo linalofaa kushughulikiwa. Nikimalizia, kama tunataka wakulima wa kahawa wawe na pesa mfukoni, lazima tuwaangalie. Katika gazeti ya Serikali juzi, kulikuwa na tolea ambalo Waziri Mbadi alisema sasa wakulima watakuwa wanatozwa asilimia 0.3 ya pesa ambazo zitaenda kwa taasisi ya CMA ambayo iko kwa Wizara ya hazina. Asilimia 0.3 itaenda kulipa malipo ya moja kwa moja inayoitwa DSS na asilimia 0.2 ambazo zinafaa kwenda katika soko la Nairobi Coffee Exchange. Hata tukiamsha Kimuri na tuendelee kutoza wakulima, itakuwa ni ubaguzi wa wakulima kwa sababu CMA inatoa pesa zake katika hazina kuu. Kwa nini mmea mmoja tu ndio utatozwa pesa na CMA? Hilo ndio swali langu. Najua hii si sehemu yako lakini ningependa ufuatilie kidogo ndio uone wakulima wako wanakatwa pesa ngapi. Kama Kirinyaga tumejipanga. Najua unakubaliana na mimi kuwa kama kuna mahali vyama vya ushirika vimekita mizizi ni Kaunti ya Kirinyaga. Tuko na viwanda 72, vyama vya ushirika 14 na chama kimoja kikubwa kinachoangalia mambo ya kahawa. Pia tumenunua mashini ya kusaga na tunajisagia wenyewe na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}