GET /api/v0.1/hansard/entries/1549090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1549090,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549090/?format=api",
"text_counter": 1016,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kama alivyozungumza Sen. Cherarkey, Kamati ya Devolution and Intergovernmental Relations itabidi iwaite mahasimu wote pamoja na Gavana wa Kaunti hiyo wiki hii ili watoe mwongozo kuhusu suala hili. Ni aibu kwamba Kaunti ya Nyamira imeshindwa kutatua masuala kama haya madogo. Nakumbuka mwaka wa 2018 tulikuwa na shida katika Kaunti ya Mombasa. Kulikuwa na watu wanaandamana kila siku kulitisha Bunge la Kaunti ya Mombasa wakisema fagia Bunge! Fagia Bunge! Tulipouliza hapa, baada ya wiki moja, gavana, na spika waliletwa hapa na matatizo haya yakamalizwa siku moja. Kwa hivyo sio masuala ya kungojea. Haya ni masuala Kamati husika inafaa kuyavalia njuga na wahakikishe ya kwamba kufikia Jumanne wiki ijayo tumepata mwafaka kuhusiana na suala hilo. Haiwezekani kaunti kupoteza wakati kwa kuwa na Mabunge mawili, Maspika wawili, Makarani wawili, Bunge moja likikaa msituni na lingine lakaa mjini. Ni aibu. Kwa hivyo, naomba Kamati hii husika ifuatilie suala hili kwa haraka ili tupate mwelekeo kuhusu ni nani anayestahili kuendesha mambo ya Bunge la Kaunti ya Nyamira kwa watu wa Nyamira."
}