GET /api/v0.1/hansard/entries/1549124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1549124,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549124/?format=api",
"text_counter": 1050,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninataka kuchangia hii Kauli ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. Omogeni. Hili ni jambo ya kusikitisha sana. Katika Kaunti ya Nyamira, kuna watu ambao wamesoma; kuna watu ambao wanaelewa kunaendelea namna gani. Kwa hivi sasa, tunaona aibu tupu ambayo huyu Gavana Amos Nyaribo ameleta ndani ya Kaunti ya Nyamira. Haiwezekani kuwe na County Assembly mbili ikiwa wewe ni gavana mmoja pale. Ni matusi kwa watu wa Kaunti ya Nyamira kufanyiwa namna hii. Juzi, alituambia ya kwamba yeye hajui ni county assembly gani ambayo iko na mamlaka zaidi ya nyingine. Lakini ikifika wakati wa kutambua pale anafaa kupeleka pesa, anaanza kuangalia mahali pesa zinaweza kuenda. Haangalii ni county assembly gani ambayo inafaa kupata pesa kulingana na sheria. Tokea mwanzo wa ugatuzi, haijafanyika hata siku moja katika Kenya hii kwamba katika kaunti moja, kuna county assemblies mbili. Je, wewe kama gavana, uko na akili kweli! Una akili kwamba unaweza kuruhusu county assemblies ziwe mbili nawe ni gavana mmoja unaketi mahali pale. Ndiyo sababu, alipokuja hapa na akaulizwa maswali, ilipatikana ya kwamba yeye mwenyewe, katika taarifa ya masomo yake, kuna shida. Alileta makaratasi gushi, ndio akaruhusiwa kugombea kiti. Hii tabia ya kuruhusu watu kuleta makaratasi gushi halafu wanaruhusiwa kugombea vyeo, hii ndiyo imetufanya sasa kuwa na magavana ambao wako na tabia kama hizi. Hawajui kazi yao kwa sababu hata kuenda shule ilikuwa shida. Huu uchawi ambao unaendelea ndani ya Nyamira ukome. Huyu gavana anafaa aitwe, aje hapa; asiende kwa kamati. Aje hapa aonekane na Bunge Zima la Seneti ili tuweze kumhoji na kumwambia atuonyeshe vizuri hizo karatasi zake za kuonyesha kwamba alienda shule; atuonyeshe hapa na tuhakikishe kwamba ziko sawa. Ikiwa haziko sawa, zipelekwe katika kituo cha sheria ama kitengo ambacho kinaweza kuangalia vyeti hivyo. Hatuwezi kuwa na mtu ambaye hawezi---"
}