GET /api/v0.1/hansard/entries/1549166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1549166,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549166/?format=api",
    "text_counter": 1092,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, naunga mkono yote ambayo ndugu yangu ambaye ni Kiongozi wa Wengi amesema kuhusu Mswada Huu. Hii ni sheria ambayo itatupa nafasi ya kufungua ukurusa mwingine ili watu wasaidike wakati kuna janga. Hii ni mojawapo ya Miswada ambayo si ya kawaida lakini inaweza kutupatia mamlaka. Wahenga walisema kuwa fimbo ya karibu ndio huua nyoka. Hii inamaanisha kuwa kitu ulichonacho ndicho hukusaidia wakati una shida fulani. Sisi tulikuwa katika shida kubwa na ilikuwa lazima tuepukane na shida hiyo. Kwa hivyo, ni lazima tuwe na sheria ambayo itatusaidia kutoka katika janga hilo. Ndio sababu nasema kuwa fimbo uliyonayo mkononi ndio itakusaidia kuua nyoka. Isije ikawa kama dau linalokusaidia kuvuka mto kisha baadaye unaliita gogo."
}