GET /api/v0.1/hansard/entries/1549168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1549168,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549168/?format=api",
    "text_counter": 1094,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Huu ulikuwa mojawapo ya misemo iliyotumika katika NADCO. Watu walikuja pamoja na kupendekeza sheria hiyo. Tukiwa katika shida ama janga lolote la kisiasa, ni lazima watu wakae ili tupate suluhisho. Hii ni mojawapo ya sheria ambazo zilipendekezwa. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unaweza kupeana uhai kwa jopo ili sheria ambayo inaweza kutumika wakati wa dharura itengenezwe. Majukumu kama hayo ni muhimu sana. Ikiwa watu wanaopatikana katika hali hiyo wanaweza kutafakari na kutoa majukumu kabla ya janga kutokea, hiyo itakuwa njia nzuri. Sheria endelevu kama hii ambayo inapendekezwa inafaa kuwa. Ikiwa itaweza kutekelezwa, basi, kutakuwa na adhabu ikiwa mtu hatafanya hivyo. Mtu ataweza kupelekwa kortini au kuchukuliwa hatua na kutakiwa kulipa faini ya shilingi laki tano. Bi. Spika wa Muda, kwa kumalizia, sheria hii ina umuhimu na vile vile ni nzuri kwa sababu itatusaidia wakati wowote. Kwa hivyo, naunga mkono sheria hii endelevu kwa sababu nilizotaja hapo awali. Asante."
}