GET /api/v0.1/hansard/entries/1549214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1549214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549214/?format=api",
    "text_counter": 1140,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia marekebisho ya Mswada wa Sheria Endelezi yaani, Statutory Instruments (Amendment) Bill, 2024. Sheria hii inapania kuadhibu wale ambao wamepewa jukumu la kutunga sheria hizi endelezi, iwapo watakosa kuzitunga sheria hizo kwa muda ule ambao umewekwa na sheria ama muda wa miezi 12 baada ya sheria hiyo kupitishwa na Bunge, na kuwekwa sahihi na Rais, ili kutumika katika nchi yetu. Kwa sasa, kuna sheria nyingi ambazo zilipitishwa na Bunge ambazo mpaka sasa hazijaweza kutumika kikamilifu, kwa sababu sheria endelezi ambazo zilipaswa kutungwa hazijatungwa. Utungaji wa kanuni hizi endelezi, mara nyingi huwa zinachukua muda kwa sababu ni jambo ambalo lazima zipitie zile taratibu zote za kutunga sheria ambazo Bunge linapitia wakati zinatungwa. Kwa mfano, lazima zipelekwe katika uhusishaji wa umma au public participation wakati sheria hizi zinatengenezwa. Vile vile, lazima iangaliwe"
}