GET /api/v0.1/hansard/entries/1549216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1549216,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549216/?format=api",
"text_counter": 1142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kwamba hazikiuki Katiba na hazikiuki ile sheria kuu ambayo imempa nafasi Waziri ama jopo linalotunga sheria hizo, kuweza kuhakikisha kwamba wametunga sheria hiyo na yale mambo ambayo yanatakikana kabla ya sheria hii kupitishwa, yote yamewekwa katika sheria. Kwa hivyo, lazima yapitiwe ndio sheria hizi ziweze kutumika. Vile vile, sisi kama Bunge, tuna muda maalum ambao lazima tuutumie ili tuweze kupitisha sheria hiyo. Ikiwa hatukuweza kupitisha kwa muda ule, sheria ile inaweza kutumika bila kupitishwa na Bunge. Kwa hivyo, suala la kuwapa muda ama kutoa vigezo vikali ambavyo lazima Waziri afanye, na iwapo hatafanya, ataadhibiwa ni jambo ambalo linatilia nguvu uwezo wa Bunge hili kuweza kudhibiti ile fursa ambayo Waziri, ama jopo limepewa kutunga sheria ambayo ingeweza kutungwa na Bunge. Jambo ambalo nimeona hapa, ya kwamba hii faini ambayo imetolewa ya Shilingi laki tano, ni kidogo sana kwa sababu, jukumu ambalo Waziri ama jopo lile limepewa ni kubwa. Kwa hivyo, lazima iambatane na ongezeko la faini hiyo. Kwa hivyo, lazima faini hiyo isiwe chini ya Shilingi millioni mbili. Tukiangalia yale mambo ambayo yamezungumziwa katika sheria hii, mengine ni mazito sana. Ilitakikana kutungwe, kupelekwe kanuni bungeni ya kuweza kuendeleza sheria hizi. Iwapo haikuendelezwa kwa mfano, serikali imeweza kupoteza fedha ambazo zingechukua kutokana na sheria hii. Kwa hivyo, kupotea kwa nafasi hizo inafaa kuambatane na faini ya juu ambayo waziri ama yule mtu anayehusika ataweza kutozwa ili aweze kupeleka sheria katika Bunge. Vile vile, kupeana nafasi kwa sababu sheria zinazoletwa Bungeni zinapitia mikononi mwa Waziri. Sheria ambazo zimetungwa na Bunge na wakatoa fursa kwa Waziri kutengeneza sheria endelezi ili kuendeleza Mswada wa sheria. Mara nyingi hawana hamu ya kupitisha sheria zile kwa sababu mara nyingi zitakwaza maswala fulani. Kwa hivyo, nafasi inayotolewa hapa kwa yule ambaye ameweza kutunga sheria ile ama yule ambaye amedhamini sheria ile kuweza kuleta sheria endelezi, ni fursa nzuri kwa vile inawapa nafasi wale ambao wanaona kwamba interests zao ama mambo yao yakiendelezwa na sheria hii, ili yaweze kuendelezwa bila kupoteza wakati. Mpaka sasa, swala la sheria endelezi zinazokwisha baada ya miaka kumi, halijaweza kuzingatiwa na mashirka mengi. Kwa mfano wiki iliyopita katika kamati ya Sheria Endelezi, maarufu, Committee on Delegated Legislation, tulikuwa tunjadili mapendekezo ambayo yameletwa na shirika la National Construction Authority (NCA) ambao walikuwa wanataka kubadilisha sheria ambazo kanuni endelezi ambazo zilikuwa zinatumika na kuleta mpya ijapokuwa zilikuwa zimekwisha mwaka wa 2023. Bado walikuwa wanataka kuzirekebisha zile ambazo zilikuwa zimeisha mwaka 2013. Miaka kumi baadaye, swala lingine ni kuwa wakati tulipoingia katika Bunge hili, zililetwa karibu kanuni 1,743 ambazo zilikuwa zimekwisha muda wa kuhudumu wa miaka kumi. Tulikataa kuzipitisha kwa sababu, sheria zile zilikuwa zinahusu wizara tofauti. Lakini wakati notisi ilipotolewa na ofisi ya mkuu wa sheria ya kwamba aliweza kuziongezea muda. Ilikuwa ni kinyume na sheria kwa sababu kila sheria ilikuwa chini ya wizara fulani."
}