GET /api/v0.1/hansard/entries/1549218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1549218,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549218/?format=api",
"text_counter": 1144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa hivyo, ilikuwa ni wizara husika waweze kuleta marekebisho haya ili waongezewe muda ndiyo waweze kuongezea sheria hizo muda. Ukiangalia katika kaunti zetu, zile sheria za ujenzi wa nyumba, nyingi zao ni zile ambazo zilikuwa zinatumika wakati kulikuwa na manispaa na mabaraza za miji. Hawajaweza kutunga kanuni mpya za kuweza kusimamia mambo ya ujenzi. Ukiangalia, majumba mengi yamejengwa upya katika miji mikuu, hata affordable housing ama zinazojengwa na serikali, lazima zipitie zile sheria za nyumba za ujenzi katika kaunti zetu. Ipo haja na ninafikiri, hili nitalizungumzia katika kamati yetu, kuangalia sheria zote za ujenzi katika kaunti zetu kama zimeweza kuambatana na sheria ambazo ziko. Je, zimeweza kuhudumu katika ule muhula wa miaka kumi ambao umewekwa na sheria ama la? Mhe. Spika, naona sehemu nyingi katika kaunti ya Mombasa, majumba yanajengwa mapya lakini ukiangalia huduma za maji, ni zile za zamani. Ukiangalia umeme ni ule ambao ni wa zamani. Tukiangalia maswala ya maji machafu, hukuna miradi ambayo yamepangwa kufanywa ili kuchukua hizi nyumba mpya ambazo zinajengwa. Kwa hivyo, utapata kwamba nyumba nyingi zinamwaga maji machafu baharini ambako zinadhuru viumbe ambavyo viko kule. Nyumba nyingi, hazina nafasi nzuri ya kuweza kupata vijana ama watoto kucheza na sehemu nyingine za kujiburudisha. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia pakubwa kudhibiti ile nguvu za Bunge katika kutengeneza sheria na kanuni za kuhudumu sheria hizi. Asante sana Mhe, Spika kwa kunipa fursa hii."
}