GET /api/v0.1/hansard/entries/1549378/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1549378,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549378/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia kauli iliyoletwa na Sen. Mwaruma. Kazi inayofanywa na machifu na wazee wa mitaa ni muhimu sana katika nchi yetu. Kwa hakika, wanafanya kazi ngumu. Kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, kuna mzee wa mtaa alipigwa risasi na kuuliwa na majambazi ambao walikuwa wanahusiana na ugaidi, yaani Al Shaabab . Familia iliondoka patupu. Mambo ambayo yanapelekwa kwa polisi na kufika mahakamani yanachukua muda mrefu kutatuliwa kuliko yale ambayo yanazungumziwa kwa chifu na kupitia kwa wazee ambao wanakaa kwa chifu, hususan maswala ya kijamii kama vile ugomvi katika ya bibi na bwana nyumbani. Kwa hivyo, Mhe. Spika, hawa ni watu muhimu sana. Hivi sasa, kwa sababu ya ukosefu wa kazi, baadhi ya machifu ambao wanaajiriwa wamefika mpaka chuo kikuu na wana shahada ya digri katika masomo na taaluma mbali mbali ambazo wamesomea. Walakini, kwa sababu ya ukosefu wa kazi, wanaendelea kufanya kazi ya chifu. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwa jamii kuwatambua hawa watu na umuhimu wao katika jamii. Mhe. Spika, zamani hata wanafunzi wa university walipokuwa wanafukuzwa lazima wangeripoti kwa chifu. Ijapokuwa chifu hakusoma, ilikuwa lazima uripoti kwake ili uone ile authority ama umuhimu wa kazi ya chifu. Kwa hivyo, ni lazima terms za kazi za watu hawa ziboreshwe ili wanapofanya kazi na majukumu ambayo wamepewa wayafanye kwa kuzingatia kwamba kazi yao inatumbulika. Juzi, Waziri Murkomen alitoa agizo kwamba, iwapo kutapatikana pombe haramu katika eneo fulani, chifu wa hiyo eneo atapoteza kazi. Hiyo sio njia ya kuwashajaisha machifu kufanya kazi. Wanafanya kazi muhimu na kazi yao ni lazima itambuliwe na vile vile, waweze kulipwa mshahara ambao utazingatia zile kazi na changamoto wanazozipata katika kazi zao. Asante."
}