GET /api/v0.1/hansard/entries/1549380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1549380,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549380/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia kauli iliyoletwa na Sen. Jones Mwaruma. Ni vizuri ijulikane wazi kwamba machifu na manaibu wao wana kazi muhimu wanayofanya. Ikumbukwe kwamba, hawa manaibu wa chifu ndio wanashughulikia mambo ya usalama pamoja na wazee wa mitaa. Kwa mfano, ukitembea Kaunti ya Laikipia, utapata machifu wengi ndio wanahusika sana na mambo ya usalama. Kwa mfano, katika eneo la Doldol, kumeuwa chifu kwa sababu yeye ndio anahusika. Ngómbe wanapoibiwa, wao ndio wako katika mstari wa mbele kufuata. Kwa hivyo, wanapaswa kushughulikiwa. Unapata chifu anatumia pikipiki yake ambayo hajapewa na serikali na mafuta yake. Chifu anatumia pesa zake na hawezi kupewa fidia na serikali. Kwa hivyo, kauli hii imeletwa na imesema ya kwamba kuongezwa kwa mamlaka ama madaraka haifuati kiwango cha masomo waliyonayo. Wengi wao, ambao ni manaibu chifu, waliajiriwa wakiwa ni naibu chifu na atastaafu akiwa naibu chifu. Hawezi kufika kiwango kingine."
}