GET /api/v0.1/hansard/entries/1549460/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1549460,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549460/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kitu ambacho ningependa kusisitiza ni kuwa tunataka kama Wakenya tupate kazi safi. Ni matumaini yetu kuwa wale watu watakaochaguliwa watatimiza wajibu wao na kufanya kazi vilivyo. Vile vile, tunajua watu ambao wanakuwa interviewed wanatoka sehemu mbalimbali za Kenya. Hii sio kazi ambayo unaweza kuketi na kuchagua watu. Tunataka kuona katika muda wanaouhitaji ili kumaliza kazi hii, watachukua watu kutoka upande zote za Kenya. Ni jambo kubwa ama jambo lililo na mzigo mkubwa katika muda huu ambao wameuliza. Kwa hivyo, mimi nataka kuunga mkono ya kuwa ni sawa wakiongezewa siku hizi 14 ambazo wameuliza. Ikiwa wamemaliza zile siku zao 90 kulingana na muda waliyopewa, ninaona tuwapatie muda zaidi. Tunajua ya kwamba Wakenya wamemaliza muda mrefu sana bila jopo hili ambalo linaweza kusimamia mambo ya kura na mipaka ya maeneo Bunge nchini. Sio kazi rahisi. Hii imefanya, kwa muda huu wote ambao hatukuweza kuchagua hawa watu, imekuwa vigumu sana kuweza kupata wabunge na wakilishi wadi katika sehemu mbalimbali ya Kenya ambao wameweza kupoteza ubunge au udiwani wao. Tunavyoongea hivi sasa, eneo bunge la Magarini katika Kilifi Kaunti, kuna mwenzetu alifanya petition mahakamani, akafaulu na tukapoteza ubunge wa ndugu yetu, Mhe. Harrison Kombe. Katika muda huo ambao watu wa Magarini wamekaa bila mbunge ni muda mrefu sana. Wamekuwa bila mbunge na kuona mambo mengi yametendeka katika nchi, ilhali wananchi walienda asubuhi kupiga kura ili wapate kiongozi wao. Kiongozi wao alitolewa na mahakama. Hivi sasa atarudi katika ukingo wa mashindano ili aweze kuchukua kiti chake tena. Ingekuwa nafasi nzuri, tuwapatie hawa nafasi ili waweze kumaliza halafu kamishma waingie ofisini ndiyo eneo la Magarini lijitayarishe kuwa na mbunge. Tuna matumaini makubwa ya kuwa ndugu yangu, Mhe. Harisson Kombe, atachukua nafasi hiyo tena."
}