GET /api/v0.1/hansard/entries/1550283/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1550283,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1550283/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Mhe. Spika, Lamu inajulikana kwa kutegemea sana utalii. Tunauza samaki sana katika eneo Bunge langu la Lamu Mashariki. Kwa hivyo, watalii wakiathirika kidogo tu, sisi pia tunaathirika. Nataka Waziri aliambie Bunge hili ni kitu gani kilitokea Mangai, ambapo Chifu alitafutwa na Al-Shabaab. Kuna Gavana aliyesema kwa jambo la vitambulisho kuwa ni vibaya watu wa Lamu wasifanyiwe vetting kwa sababu Al-Shabaab wanaingia nchini. Kwa hivyo mimi na watu wangu tuna wasiwasi hao watu wasifanye kusudi to justify their point . Kwa hivyo, Waziri atuambie ni nani alihusika kumtafuta Chifu Mangai. Kama ni Al-Shabaab utuambie, maanake walikuja kwa njia tofauti kabisa. Eti Al-Shabaab walikuja, wakaongelesha watu, wakawapa tende, kisha wakaondoka. Tuambie ni kina nani waliofanya hivyo. Inatuathiri sana kwa sababu uchumi umeharibika Lamu. Leo tuambie kinagaubaga ni hao kina nani, kwa sababu sisi tunashuku hao magavana ambao hawataki sisi tupate vitambulisho pengine ndio waliofanya kusudi to justify their point . Asante. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}