GET /api/v0.1/hansard/entries/1550285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1550285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1550285/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kwanza nampongeza Waziri kwa sababu alipokuwa katika Wizara ya Uchukuzi, alifanya kazi safi sana. Mhe. Spika, niruhusu niulize swali ambalo limenisumbua sana. Ndani ya Kaunti ya Mombasa, tumekuwa na ukosefu wa usalama. Vijana wadogo, kama ulivyosema wa miaka 12 hadi 19, wameshika vipanga wanakatakata watu. Juzi waliingilia watu pale Makadara Grounds wakati wa Ramadhan. Kisha tulipokea cruise ship ya watalii. Watalii walikuja Mombasa wakatuletea pesa hapa Kenya. Lakini wale vijana waliwaibia vipochi vyao, na wakawapiga mpaka watalii wakaamua kugeuza meli ikarudi kwao nyumbani. Kwa sababu ya hilo, hapo tumeukosa mtaji ndani ya taifa hili. Juzi pia kule Likoni, tuliona ‘Wajukuu wa Bibi’ waliokuwa wengi wakiwakatakata watu kwa mapanga. Mchana huwezi kutembea; usiku huwezi kutembea. Waziri, nataka utuambie vile utatusaidia Mombasa ili tuweze kuwatoa hapo. Nimeona Kwale mumeshika watoto mpaka na wazazi wao. Je, Mombasa mumetupangia kitu gani, maanake hili limekuwa donda sugu? Asante sana Mhe. Spika."
}