GET /api/v0.1/hansard/entries/1550287/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1550287,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1550287/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia fursa hii ili nitoe hisia zangu, na nimuulize Mhe. Waziri maswali. Kwanza, nampatia kongole kwa kupata Wizara hii. Najua ni mtenda kazi, na atawatendea watu wa Kenya kazi hii. Kila Wizara unayopewa unawajibika kwa kufanya kazi yake. Kuna suala la locations ambazo zilikuwa gazetted. Kuna locations Kwale ambazo zilikuwa gazetted mwakwa wa 2017 kama Msambweni, Matuga, Kinango, na Lunga Lunga. Mpaka sasa hivi, bado hatujapata machifu na manaibu wao. Serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha watu hawa wameajiriwa ili wawajibike kuwafanyia kazi watu wa Kaunti ya Kwale? Pili, Mhe. Spika, nazidi kulitilia pondo lile suala la vijana wa vipanga, ambalo limekithiri pale Kwale County katika sehemu ya Ukunda. Askari wanajaribu kilithibiti, lakini tunahitaji nguvu zaidi ya kukabiliana na suala hili. Tunajua ni suala ambalo linaathiri pakubwa…"
}