GET /api/v0.1/hansard/entries/1550726/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1550726,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1550726/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika nikimuunga mkono ndugu yangu, Mhe. Martin, ningependa kusema kuwa kama vile kampuni za sukari, imekuwa dhahiri kuwa Wakenya wengi wanaofanya kazi katika hizi kampuni wanadhalilishwa sana haswa katika suala la kujiunga na labour unions . Haya ni mambo yametokea mahali kwingi kama vile Mombasa na EPZ. Viza kama hivi tumekumbana navyo. Kwa mfano, wafanyikazi hao wanapotaka kujiunga na unions, wanazuiliwa ilhali hii ndio njia pekee watakaotumia kutatua hayo matatizo. Mshahara wao ni duni kabisa sio vile sheria ya labour ilivyo. Pia, hawapewi vifaa au zana za kuwawezesha kukabiliana na changamoto zilizopo kazini mwao. Wengine, kama ulivyosikia, wanalipwa kupitia M-Pesa. Sasa mfanyi kazi atajiuliza hatma yake iko wapi? Mtu anapopata tatizo kubwa, anashindwa atasaidika vipi ilihali hana union . Shirika la NSSF pia limeondolewa, hawalipiwi. Kwa hivyo, kwa maoni yangu, ijapokuwa hao wafanyakazi walishiriki kwenye maandamano, wamedhulumiwa sana na wanastahili kupata haki kupitia hili Bunge na haswa, kamati inayohusika na maswala haya. Tunaomba kamati husika iangalie kwa kina na kuhakikisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}