GET /api/v0.1/hansard/entries/1551286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1551286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1551286/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Naibu Spika. Naunga mkono taarifa ya Seneta wa Nyeri, Sen. Wamatinga, kuhusu mashamba ya KEVEVAPI. Mimi ni naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo na ningeomba Kamati hii ipewe nguvu ya kuangalia vile mambo ya mashamba imeleta shida. Hii shida haipatikani kwa mashamba ya KEVEVAPI pekee, lakini ni Kenya nzima. Wale matajiri ambao wana hela nyingi, wanapopita mahali na waone shamba ya serikali, mtu binafsi ama ya familia ambayo haijiwezi, wanaleta shida. Tume ya National Land Commission (NLC) haifanyi kazi vile inapaswa kufanya. Utapata kwamba kama koti imetoa uamuzi kwamba shamba ni ya KEVEVAPI, unapata NLC ikisema kuwa mambo hayo sio sawa. Unapata kwamba Kenya nzima kuna mvutano wa hapa na pale. Ningeomba tutunge sheria ambayo itahakikisha kwamba mtu yeyote ambaye atavamia mashamba ya serikali, hata kama ametumia pesa zake kufanya hicho kitendo, apelekwe kotini na afungwe maisha. Mambo ya mashamba katika Kenya nzima imeleta shida. Kwa hivyo, naunga mkono huu mjadala kuhusu mashamba ya KEVEVAPI. Kama mnavyojua, KEVEVAPI inahusikana na mambo ya mimea na vitu vingi na huku mashamba yao yanaendelea kuchukuliwa na matajiri. Asante."
}