GET /api/v0.1/hansard/entries/1552930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1552930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1552930/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Kabla niulize swali langu niruhusu nitoe pongezi kwa Serikali hususan, Wizara ya Uchukuzi na Barabara kwa kuruhusu ndege za kimataifa za Uturuki na Qatar, kuweza kutua moja kwa moja kwa kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Moi. Tarehe 26/8/2024 nilisimama na kupeana ombi ya kuruhusiwa kwa ndege hizo za kimataifa kutua katika kiwanja kile. Ni pongezi. Swali langu kwa Bw. Waziri ni kwamba kuna mikakati gani ya kuboresha kwa viwango vya kiwanja kile ili kiweze kuwa na muonekano kimiundo msingi kwa sababu wale wageni tunaowatarajia katika kiwanja kile sasa watakuwa ni wa kitalii. Wamezunguka katika mataifa mengine ya nje na wameona mionekano mizuri. Je, kuna mikakati gani ya kuweza kuona kwamba uwanja huu wa ndege wa Moi umeboreshwa na kupata muonekano mpya unaoenda sambamba na viwanja vingine vya kimataifa? Waswahili husema, kicheko chataka meno. Je tumejipanga sawia kuona kuwa tutakapokuwa tunawapokea, wataona hali tofauti na ile waliyoiacha hapo awali? Asante, Bw. Spika wa Muda."
}