GET /api/v0.1/hansard/entries/1552943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1552943,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1552943/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mandago",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13577,
"legal_name": "Kiplagat Jackson Mandago",
"slug": "kiplagat-jackson-mandago"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Swali langu kwa Bw. Waziri ni Serikali ina mipango gani ili kupanua runaway ya Eldoret International Airport na pia kukarabati airstrip ya Baringo County ambayo inatumika sana kwa mambo ya masuala ya usalama kule Kerio Valley? Ningependa kujua kwa sababu hii imekuwa kwa mipango ya Serikali kwa muda mrefu kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Eldoret utapanuliwa ili uchukuzi wa bidhaa za kilimo uboreshwe. Bw. Spika wa Muda, unavyoelewa, Kaunti ambazo zinazunguka Mji wa Eldoret ni kaunti ambazo uchumi wao unategemea kilimo sana. Kwa hivo, tungependa Waziri atueleze kama kuna mipango ya Serikali ya mwaka wa matumizi ya fedha wa 2025/2026, kupanua huo uwanja wa Eldoret Airport ili sisi kama wakulima tuiitumie? Vile vile, airstrip ya Baringo ambayo inahusika sana na mambo ya usalama na inasaidia sana wakati tunakuwa na majeruhi Kerio Valley kwa sababu ya mambo ya usalama, maofisa wetu wa usalama na pia raia wanasaidika kupata huduma ya kwanza na ya haraka kwa mambo ya matibabu."
}