GET /api/v0.1/hansard/entries/1553139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1553139,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1553139/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "maafisa wakuu wa idara tofauti katika gatuzi hilo. Ni jambo la kuvunja moyo kama Kaunti ya Isiolo itakaa kwa zaidi ya miezi miwili bila ya maafisa wakuu, kwani ndio wanaoshughulikia utenda kazi katika gatuzi lile kila siku. Gavana wa Kaunti hiyo amekuwa na shida kila wakati. Kwa hivyo anafaa kutilia mkazo jambo hili. Hatuwezi kugawa pesa za ugatuzi kama Seneti, lakini Kaunti ya Isiolo haina maafisa wakuu wanaopaswa kutenda kazi. Hii itapelekea gatuzi hilo kubaki nyuma na kuwa na shida nyingi baadaye. Inawezekana Gavana ana mpango wa kufuja pesa za Kaunti ya Isiolo. Kuhusu suala la Nyamira, sikuweza kufuatilia walipokuja Seneti lakini nilifuatilia kwa runinga. Niliona kikao cha Bunge la Nyamira wanachokiita Bunge Mashinani. Waliiga tunavyofanya Seneti, lakini waliiga visivyo. Hauwezi ukagawanya Bunge la Nyamira kuwa mabunge mawili. Hilo si jambo la kufikiria. Namwomba Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi Seneti afuatilie jambo hili. Nilikuwa mwenyekiti kwa miaka miwili muhula uliopita lakini hatungekubali jambo kama hili litendeke kwani tutakuwa tumezembea katika kazi yetu kama Seneti. Tuache kumuekelea mzigo Seneta wa Kaunti ile peke yake. Tunapaswa kusimama wima na kidete na kusema kuwa haiwezekani kugawanya Kaunti ya Nyamira mara mbili. Tutalaumiwa sio tu na watu wa Nyamira, bali na Jamhuri ya Kenya kwa sababu kazi yetu kubwa ni kutetea na kulinda gatuzi zetu. Inaonekana tayari tumelemewa kwani nasikia fununu kuna kaunti moja ambayo watu wamegawanyika. Pesa tunazotuma kwa Bunge la Nyamira zinalipwa nani? Tunapaswa kujiuliza swali hilo gumu. Hatufai kungoja mahakama ituambie tutakavyofanya. Hii ni kazi yetu. Tunapaswa kuifanya kwa ueledi na ustadi bila kuogopa. Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hiyo."
}