GET /api/v0.1/hansard/entries/1553725/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1553725,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1553725/?format=api",
    "text_counter": 303,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika. Hizo shule ambazo zimejengwa kwa ajili ya wanafunzi wa Gredi 9, 10, 11 na 12 bado hazina maabara. Pia, kuna shule za sekondari ambazo hazikuwa na maabara ya kutosha. Baadhi ya shule hizo zinakuja kwa ofisi yangu zikiomba nizijengee. Hata zile ambazo zina maabara, hazina vifaa vya kutumia katika maabara hayo ipasavyo. Je, Waziri anafanya nini kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata huduma hizo shuleni?"
}