GET /api/v0.1/hansard/entries/1554092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1554092,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1554092/?format=api",
"text_counter": 670,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. ZamZam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "… Yaani ukiangalia vile anavyokwenda katika maisha yake… Nilimjua nikiwa pale ODM. Nilipoenda kujiandikisha kama mwanachama wa ODM kwa mara ya kwanza, nilimpata pale ofisini. Alinikaribisha kwa furaha, akanipa nguvu na kuniambia kuwa nisijali hata kama nimetoka katika sehemu ambazo pengine wanawake bado hawajachukuliwa vizuri. Lakini kwa uweledi wangu, aliona kuwa nina uongozi ndani yangu. Alisema kuwa ana imani kuwa nikipata kiti hicho, nitaiweka Mombasa juu. Maneno yake yalinipa ujasiri na ndio maana mnaniona katika Bunge hili. Nikizungumza, watu wanasikiza na Mombasa inafurahi. Ninafanya kazi kule Mombasa ili nisimuangushe. Alitupea nguvu sisi wanawake ya kufanya kazi na kuamini kuwa sehemu ya mwanamke si jikoni tu. Mwanamke pia anaweza kuwa ndani ya boardroom na kutoa maamuzi mazito ya taifa. Kwa hivyo, ninampigia upato sana na kumuombea Mungu katika hii nomination yake. Najua ameshapata cheo hicho maanake kama tunapitisha jina lake, ataleta mawazo mazuri katika kujenga taifa la Kenya. Kwa hivyo, ninampea support kama Mama Kaunti wa Mombasa, na kumwambia aendelee kuwainua wanawake."
}