GET /api/v0.1/hansard/entries/1554616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1554616,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1554616/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii nami nizungumzie tamthilia ya watoto wa Butere. Akili za hawa watoto zinanasa mambo mengi sana. Katika shule nilikuwa nafanya tamthilia. Vitabu vingi vimeandikwa. Mifano ni “Mashetani” na “Kusadikika”. Niliangalia ule mchezo nikaona wanasiasa wameingia ndani ya tamthilia ya hawa watoto. Wanasiasa wameingia wakawa wanatoa uwazi wa maneno. Sisi tunajua Kenya inateketea. Kuna wakati tumetoka hapa mbio kwa sababu ya mambo ambayo hayakuwa sawa. Kwa hivyo hatuwezi kukubali watoto wetu wadhurike akili. Watoto wapewe michezo mingine. Kuna michezo mingi. Maneno ya kutumia pia yako tofautitofauti. Lakini, nikiangalia ule mchezo, ulikuwa umeingia siasa na nia tofauti ilhali wale watoto wako innocent na hawaelewi wanaambiwa wafanye nini. Kwa hivyo, katika shule zetu, tuhakikishe kwamba walimu wanawekea watoto wetu mambo yatakayopatia akili zao kunasa mwongozo mzuri, na si mambo ambayo yataleta utatanishi na mfarakano katika taifa. Hivyo, nasema ile ban iko sawa. Nilicheza tamthilia. Watoto wapewe mchezo ambao unaweza kuwa na mafunzo mazuri. Wasipewe michezo ambayo itakuja kuchoma taifa. Asante sana."
}