GET /api/v0.1/hansard/entries/1554968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1554968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1554968/?format=api",
    "text_counter": 432,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Najua muda umetupa kisogo lakini kwa sababu huyu ni kiongozi mama, nataka niweke sauti yangu. Kwanza, namshukuru Mhe. Rais kwa kutambua ya kwamba kina mama ni viongozi na wanatakiwa wawe katika nyanja, haswa zile za kufanya maumuzi katika taifa letu la Kenya. Dadangu Regina Akoth ni mama ambaye amefuzu katika viwango vya juu sana katika tajiriba ya elimu. Tukiangalia uzoefu wa kazi haswa katika taasisi za umma, amekuwa na uzoefu wa hali ya juu sana. Amependekezwa kuongoza biashara katika taifa letu la Kenya. Ataweka natija ya hali ya juu sana. Jana tulipitisha uteuzi wa Mhe. Judy Pareno kama mama; leo tunamzungumzia Jane Kere na Regina Akoth. Kwa zile tajiriba zake na uzoefu wa kazi na elimu yake, naamini Regina ataboresha biashara zinazohusu taifa letu na zile zinahusu mataifa mengine yakishirikiana na taifa letu, ili tujenge uchumi wetu. Pia, tutazingatia biashara za kiulimwengu. Kuna biashara nyingi sana haswa pale kwa"
}