GET /api/v0.1/hansard/entries/1554970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1554970,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1554970/?format=api",
    "text_counter": 434,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "s, zile sehemu ambazo zimetengwa ili tuweze kupata biashara za kuboresha uchumi wetu na kuleta ajira kwa vijana wetu. Regina atashirikiana na Waziri kuona kwamba hizi biashara zimeboresha uchumi wetu na zimejenga ajira, ndiposa tusikuwe na dukuduku la vijana wetu wachanga wanaosema Kenya hakuna ajira na hivyo basi wanaenda katika mataifa tofauti. Wizara hii pia inahusika na mambo ya viwanda. Kule Pwani tungependa kuwa na viwanda kama vya mnazi, korosho na biksa. Vikiwa pale, tutapata biashara kubwa. Tutaweza kupeleka korosho nje na kutengeneza bidhaa tofauti tofauti ambazo pia zitaleta fedha katika taifa letu la Kenya. Mbali na kuangalia mambo ya kimataifa, hapa kwetu Kenya pia, aweze kuwapatia nasua makundi yaliyotengwa ama makundi ya kuzingatiwa kama kina mama, vijana na wale walio na ulemavu. Makundi haya yakichukua mkopo kutoka kwa Sacco, wapatiwe nasua na mwelekeo wa biashara wanaoweza kuekeza ili wafaulu kujijengea ajira na kujenga uchumi wa taifa letu ili Kenya inawiri na itoke kati ya mataifa maskini na ijiunge na mataifa yaliyobobea. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}