GET /api/v0.1/hansard/entries/1555019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1555019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555019/?format=api",
"text_counter": 483,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Nampongeza ndugu yangu Rahim kwa kuleta Hoja hii inayokusudia kusaidia wanaougua maradhi ya saratani kupata matibabu kwa kutumia teknolojia mpya. Ndugu yangu Mhe. Rahim, anajua kwamba mna wagonjwa wengi wa saratani huko Meru. Nakupongeza kwa kuleta huu Mswada uwe msaada kwao. Naambia watu wa kule kwamba wamepata kiongozi anayewajali sana. Pia, tuangalie vinavyosababisha hii saratani. Kuna wakati tulizungumza kuhusu kemikali zinazoitwa cathine na cathinone ambazo zinatokana na mmea wa miraa. Ndugu yangu Mhe. Rahim, hata katika Kaunti ya Mombasa nimeona watu wengi wanaotumia miraa wakiathirika sana na maradhi ya saratani. Ni kwa sababu ya hizo kemikali, na si kwa sababu nyingine. Ni lazima tuambiane ukweli tunapozungumza masuala ya afya. Kenya nzima itaangamia tukificha sababu za saratani. Kuleta teknolojia katika matibabu ni vizuri na tunasema asante sana. Hata hivyo, kuzuia ni bora kuliko kutibu. Wananchi waangalie na kupunguza matumizi yao ya mimea kama miraa na mengineyo. Hii ndio sababu kubwa ya saratani kule Meru. Ninyi wenyewe mmeona na kusema kwamba saratani iko kwa wingi kule. Kwa nini? Kwa sababu mmea huu unapandwa sana huko. Pia, kuna kemikali tunazokula kwenye chakula. Akina mama pia wanapata maradhi hayo. Ninaunga mkono kuletwa kwa teknolojia hii ili isaidie kutibu akina mama na hasa wazee. Tumalize kabisa mambo ya saratani katika taifa hili. Waambiwa mficha uchi hazai. Ndiyo maana tunaambiana ukweli. Kama saratani ingekuwepo kwa wingi kwetu, hata mimi ningesema kwamba sababu kubwa ni kitu fulani."
}