GET /api/v0.1/hansard/entries/1555188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1555188,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555188/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika. Kwanza ningependa kujiunga nawe katika makaribisho yako uliyowakaribisha ndugu zetu kutoka Kilifi, hususan familia ya Mhe. Chokwe. Tunaelewa kuwa Chokwe alikuwa Spika wa kwanza wa Seneti katika taifa la Kenya. Hii ni familia ambayo inajulikana sana kule Kilifi na imejitolea mhanga kuona ya kuwa watu wa Kilifi wamepata haki yao. Zaidi sana, hawa ndugu zetu wakiwa hapa, wamejionea vile Seneti inavyo fanya kazi. Natumai kuwa wakirudi nyumbani, watakuwa na mambo ambayo wanaweza kuwaeleza ndugu zetu kule nyumbani. Nikiwa hapa kama Seneta wa Kilifi, ninawakaribisha, wajihusishe na waone wakiwa huru. Waone wakiwa mahali ambapo ndugu zao wako. Kwa hivyo, karibuni sana ndugu zangu kutoka familia ya Chokwe. Asante, Bw. Spika,"
}