GET /api/v0.1/hansard/entries/1555584/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1555584,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555584/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kuna fursa hii ili nichangie kuhusu Mswada huu wa Sen. Gloria Orwoba. Kwanza, ningependa kumpongeza sana Sen. Gloria Orwoba, kwa sababu yeye ni Seneta mteule lakini tunaona kazi anayoifanya hapa Bungeni. Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu nimemuona kwa mabango katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, akiashiria kwamba yeye ni mkereketwa mkuu wa swala hili. Vile vile, Seneta huyu amefika hapa Bungeni akiwa amevalia nguo iliyokuwa na rangi nyekundu kwa sehemu zake za siri. Kumbe ilikuwa ni ishara kwamba alikuwa anamchakato wa kuhakikisha kuwa ameleta Mswada huu ambao ni wa maana sana katika nchi yetu. Ningependa kumpongeza sana kwa Mswada huu. Vile vile ningependa kunakili semi za Sen. Eddy Oketch kwamba kumekuwepo ama kunayo sheria tayari kuhusu swala hili. Walakini, ningetaka kumueleza kwamba nimeona sheria hii imeweza kunukuu kipengele fulani cha 18 cha Sheria ya Basic Education Act na hiyo ni kuonyesha kwamba Sen. Gloria amepiga msasa sheria ambazo zipo kwa sasa kuhusu swala hili la visodo. Bi. Spika wa Muda, wanafunzi wetu wa kike, hasa wale wanaotoka mashinani, wameteseka. Ukiangalia zile sehemu za ndani za nchi hii, kama Kaunti zetu za North Eastern, kwa mfano, kaunti za Wajir, Marsabit na hata Kaunti yangu ya Kwale, kuna sehemu za ndani kama vile Shesheni, eneo Bunge la Lungalunga, Ngathini, eneo Bunge la LungaLunga na Kaza Moyo, eneo Bunge la Kinango. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}