GET /api/v0.1/hansard/entries/1555585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1555585,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555585/?format=api",
    "text_counter": 445,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hizi ni sehemu ambazo wanafunzi wetu wa kike wakifika wakati wa mwezini na hawajapata fursa ya kupata visodo, inakuwa hali ngumu kwao kuenda shuleni. Inakuwa hali ya aibu zile siku mbili au tatu ambazo wanapitia hali ya maumbile yao ya kiubinadamu. Inakuwa dhiki na aibu kwao. Inafika wakati wanatumia hata vitambara ili kuhakikisha kwamba wameweza kuzidhiri siku zao za mwezi kibinafsi. Ikiwa sheria hii itatekelezwa na ukweli tutapata fursa ya Serikali Kuu na serikali zetu za ugatuzi kuhakikisha kwamba visodo vinasambazwa katika kila shule ya upili ama ya msingi ili wanafunzi wetu wa kike wavipate. Itakuwa hali ya afueni kwao kwa sababu kwa sasa ni aibu sana kwa mwanafunzi yule hawezi kupata visodo. Sio kwamba hawana uwezo. Wakati mwingine, utapata familia zingine kule mashinani wana uwezo lakini kufikia hizo visodo ni hatua na inakua bei ghali sana na wanashindwa kuzipata. Kwa hivyo, nampongeza sana Sen. Gloria kwa hili wazo lake la kuhakikisha kwamba Serikali ime chukua jukumu la kuhakikisha kwamba visodo vimesambazwa katika kila kona na shule ya nchi ili yule msichana ambaye anahitaji visodo apate haki yake, pasipo kumjua mtu yeyote, au kuenda kwa ofisi, either ya mzee wa mtaa, chifu ama mbunge. Sisi wanasiasa tunatumia swala hili kufanya siasa. Sio vyema kwamba unamdhalilisja mtoto wa kike ili ufanye siasa yako. Ikiwa wewe ni kiongozi na unahitaji kusaidia jamii kwa kuwapatia wanawake wetu visodo, tunakuomba ufanye vile kwa njia ambayo inastahili, wala sio kuwatumia wasichana wetu kufanya siasa. Vile vile, ningependa kumpa Sen. Gloria mawazo kwamba, tumeona ameweka kamati mbili katika sheria hii. Kamati hizo zimepewa nguvu za ajabu sana ya kwamba wao ndio watasimamia suala hili lote, kuanzia kupata fedha, kufanya mipangilio na usambazaji wa hivyo visodo. Namuomba aangalie hapo maanake tunajua kwamba fedha ikitoka kwa Serikali Kuu ikienda kwa Kamati ambayo tunaona kuwa imeteuliwa na watu binafsi, hatujui uwajibikaji utakuwaje katika kamati hiyo. Vile vile, magavana wetu watakua na hali ya atiati kuipatia kamati ya kaunti kufanya kazi hii ya kusambaza visodo kupata fedha hizi. Tunajua hali ya kiuchumi ni ngumu. Nimeona ile kamati ni lazima ipate aidha allowance ama kiinua mgongo fulani ili wafanye kazi hii. Kwa hivyo, Sen. Gloria, nakuomba uangalie suala hili, Vipengele vya 12 na tatu. Hizo kamati ni nyingi, na vile vile zina majukumu ambayo ni ya nguvu sana na inaweza kukupatia shida na viongozi wengine. Bi Spika wa Muda, tayari, akina mama wetu ambao ni women representatives wana mfuko ambao unaitwa the National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). Ningependa kukutaarifu kwamba mimi nilikuwa mratibu mkuu wa kwanza kusimamia fedha hii katika Kaunti ya Kwale, wakati ambapo kiongozi wetu alikuwa Mhe. Mwenda zake marehemu Zainabu Kalekye Chidzuga, Mwenyezi Mungu amrehemu, amsamhehe dhambi zake, na amuweke mahali pema, palipo na wema. Tulifanya miradi kama hii lakini hakukuwa na sheria. Ilikuwa tu, mtu au kiongozi anaamka na kusema leo naomba nisambaze visodo. Wewe kama mratibu mkuu huna budi ila kuhakikisha umetafuta fedha na umeziweka katika ule mradi na huo mradi umefanyika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}