GET /api/v0.1/hansard/entries/1555586/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1555586,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555586/?format=api",
    "text_counter": 446,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Leo hii, tunaona sheria ya NGAAF iwehakikisha kwamba women representatives wetu wamepewa fursa ya kutafuta hivi visodo na kuvisambaza nyanjani ili wanafunzi wetu wafaidike na hivi visodo. Najua viongozi hapa watasema mbona tayari kuna sheria kuhusu visodo, kwa nini tulete sheria ingine kupitia Sen. Gloria Orwoba. Ningependa kuwataarifu kwamba hata kama hio sheria ipo, bado lile jukumu la kuhakikisha wanafunzi wetu wamepata visodo wote sawia, kila mmoja bila kubagua au kujulikana, haijaweza kutekelezwa vilivyo. Hivyo basi, ningependa kumuomba Sen. Gloria kupitia sheria hii, azungumze na hao viongozi wengine wakiwemo women representatives kwa sababu ikifika kule Bunge la pili, wanaweza kuleta shida na sheria hii. Hata hivyo, Sen. Gloria, nina imani kwamba, mkizungumziana tutapitisha sheria hii na itaweza kumuokoa yule mwanafunzi ambaye hajui lolote na yeyote, na ni mchochole, aweze kupata visodo hivi na kuendelea na majukumu yake kukaa shule afanye mitihani yake na ahitimu. Mwisho wa siku, inshallah tumuone katika Bunge kama hili pia yeye akizungumzia masuala ya wanawake wenzake. Kwa hayo, nampongeza Sen. Gloria kwa Mswada huu na ninauunga mkono. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}