GET /api/v0.1/hansard/entries/1555792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1555792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1555792/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "na Statements nyingi kwenye Bunge. Nina imani kuwa watu wake pia haswa kule mashinani watamkosa sana kwa sababu alikuwa kiongozi mchapa kazi. Ila ushauri wangu kwa ndugu yangu Mhe. Ruku ni kuwa, mwenzako aliyetoka pale tulimwingiza vizuri lakini akafanya kiburi. Hivyo tunakuomba kwa kuwa umekuwa nasi hapa na unaelewa matatizo ya wakenya hivyo ukiingia pale, uwe na heshima na adabu. Ikiwa itatokea kuwa unataka kuondoka, utoke kwa heshima ambayo umeingia nayo. Inatamausha sana ikiwa waziri amechaguliwa na kuingia kwenye serikali anaanza kutoa siri za serikali. Tunasema “siri kali”, kwa maana siri ambazo ziko kule lazima wewe uziache kule hata kama unaondoka. Ni aibu kwamba waziri ambaye alikuwa anaheshimika anaweza kutoka nje akaanza kuelezea mambo ambayo hakuweza kutuambia akiwa waziri. Ndugu yangu Mhe. Ruku, najua wewe ni mchapa kazi na una heshima. Weka matakwa ya wakenya mbele, fanya kazi kwa bidii na Mwenyezi Mungu akutangulie mbele. Nikija kwa dadangu Bi. Hanna Cheptumo, Mhe. Spika wa Muda, huyu ni mama ambaye ameingia kwenye ujane na ametoka kwenye misukosuko. Najua kuwa amefanya makosa mahali kwa kutoa matamshi yale lakini kama Mama Mombasa County, namuombea msamaha hapa kama mama ambaye pia anaelewa matatizo wanayopitia wajane. Namwambia kuwa, tumekawia kupata waziri kwa muda mrefu katika hii wizara yetu. Nawe dada yetu Hanna Cheptumo ukiingia kule, angalia masuala ya wanawake, femicide na mambo ya gender-based violence yamekuwa donda sugu katika taifa hili. Wewe kama mama, twataka utoe mwelekeo mzuri. Najua katika docket yako, kuna Principal Secretary Anne Wang’ombe anayefanya kazi nzuri sana. Ikiwa mama hataelewa mambo atakayoyapata, mdogo wake atamuonyesha vile ambavyo mambo yanavyofanywa hapa na pale ili aelewe. Kama alivyosema mwalimu wake, dada yetu, Mhe. Gladys Boss, Hanna anapaswa kuomba msamaha kutoka kwa akina mama na Wakenya kwa sababu matamshi yake hayakuwa mazuri. Hata hivyo, haimaanishi kuwa hawezi kufanya kazi. Alijibu maswali mengine vizuri na nina imani kuwa atakapozingatia masuala ya sisi akina Mama 47 wa Kaunti, atatushika mikono ili tuweze kupigana na matatizo yanayowamaliza akina mama katika taifa hili. Akina mama wengi wamekufa. Wengine wametupwa kwenye mashimo. Watoto wetu wameuwawa katika AirBnB. Wote hawakuenda kutafuta pesa kama alivyosema. Wengine waliuwawa na wachumba wao walioingiwa na ubaya mioyoni mwao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}