GET /api/v0.1/hansard/entries/1556035/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1556035,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556035/?format=api",
"text_counter": 431,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nami pia naunga mkono Hoja hii ya uteuzi wa kijana wetu Aden Abdi Millah. Namshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Kenya pamoja na Mhe. Raila Amollo Odinga kwa kufikiria kabila ama jamaa ambazo zimetengwa. Tuliona Fikirini kutoka huko Pwani. Tulimwona Profesa Shaukat kutoka Pwani. Leo tumeona kijana wetu Michael kutoka Samburu. Sasa hivi tuko na kijana Abdi. Jamani, lazima chenye sifa kipewe sifa. Nasema kwamba ubaharia na ubahari ni muhimu hususan kwa watu wa Pwani. Namjua kijana huyu kwa uzoefu wake wa elimu na kufanya kazi katika taasisi za umma na taasisi za kibinafsi. Atasaidia hata mambo ya uvuvi kule Pwani na ziwa letu la Victoria. Atasaidia pakubwa sana. Pia nimeona ni mtu ambaye amesaidia jamii kwa kiwango kikubwa sana. Tajriba yake, haswa ya elimu, itamwezesha kuleta mageuzi katika sera na katika sheria zile ambazo zinatakikana kupigwa msasa. Pia itahakikisha ubaharia na mambo ya bahari kwa jumla yameleta tija. Ataweza pia kugeuza uchumi wa taifa hili haswa tukiona kwamba kilimo samawati ni kilimo ambacho Serikali ya Kenya Kwanza imekipatia kipaumbele. Ni Serikali ya mseto sasa. Imechanganyika. Kwa hivyo, mimi ninasema kijana huyu anaweza na anatajiriba ya kuleta mageuzi ambayo yataleta tija katika mambo ya ubaharia. Naunga mkono Mhe. Spika wa Muda."
}