GET /api/v0.1/hansard/entries/1556206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1556206,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556206/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Bw. Spika. Ninaunga mkono taarifa hii iliyoletwa na ndugu yetu, Sen. (Prof.) Tom Ojienda, ambaye ni wakili mkubwa humu Kenya. Yeye pia ni Seneta wa Kaunti ya Kisumu. Taarifa yake inahusu hali ya usafi ama utumiaji wa maji katika Kaunti ya Kisumu. Ningependa kusema ya kwamba miji mingi nchini Kenya inahitaji usafi wa hali ya juu. Usafi unafaa kuzingatiwa na kaunti. Tumeona ya kwamba kaunti ambazo zinahusika huwa hazizingati vile uchafu unaweza kutupwa ama kutumika ndiposa waweze kuweka mazingira ambayo hayasababishi magonjwa. Tumekuwa na magonjwa mbali mbali. Hivi sasa kumezuka Influenza ambao ni ugonjwa mbaya. Huo ugonjwa uko kama Covid-19. Kwa hivyo, Statement kama hii inapaswa kuzingatiwa zaidi na Kamati ya Afya. Tunawaomba walete mwelekeo ambao kaunti zetu zinaweza kuzingatia hali ya usafi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services, Senate."
}