GET /api/v0.1/hansard/entries/1556241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1556241,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556241/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Abass, ambaye ni Seneta wa Wajir, kuhusu Uwanja wa Ndege wa Wajir. Uwanja wa ndege ukisimamiwa na wanajeshi inaleta hali ya sintofahamu kwa sababu wananchi wa kawaida wanapata ugumu wa kusafiri. Kabla ya uwanja huo kuchukuliwa na wanajeshi, kuna watu wetu ambao walikuwa wanautumia. Kwa sasa, ni watu wachache tu ambao wanautumia. Kuna basi moja pekee linalomilikiwa na KAA kusafirisha watu katika uwanja huo. Pengine wangefuata kilichotendeka Lanet kule Nakuru wakati Mji wa Nakuru ulipandishwa na kuwa Jiji. Waligawanya Uwanja wa Ndege wa Nakuru mara mbili ili kuwe na sehemu wa wanajeshi na sehemu nyingine kutumiwa na wananchi wa kawaida. Hii ni kwa sababu sheria zinazotumiwa na wanajeshi ni ngumu ambazo wananchi wa kawaida hawazielewi. Sheria za wanajeshi si kama za maafisa wa polisi ambao wanajua jinsi ya kuishi na wananchi wa kawaida. Bw. Spika wa Muda, napendekeza kuwa kamati ambayo itashughulikia Kauli hii izingatie kuwa na migao miwili katika uwanja ule kwa sababu ni mkubwa. Kunafaa kuwe na sehemu ya raia na nyingine ya wanajeshi ili wafanye kazi yao. Vile vile, Bw. Spika wa Muda, ningependa kuchangia Kauli iliyoletwa na Sen. Okenyuri kuhusu watu kupata makao. Inapaswa Kauli hiyo iangaliwe vizuri na kuwe na mikakati tosha ili mtu asipokuwa na makao, ijulikane anaishi wapi kabla ya kupewa mahali pa kuishi. Makao hayo yanapaswa kupeanwa bure bila mtu kulipa chochote kwa sababu watu hao ni masikini hohe hahe; hawana mbele wala nyuma. Kazi kuu ya Serikali ni kupatia watu makao na kulinda maisha yao na vile vile kile walichonacho. Kwa hivyo, naunga mkono Kauli iliyoletwa na Sen. Okenyuri. Tunapaswa kuwa na mikakati ambayo itatumiwa ili watu kupewa nyumba. Kulingana na Kauli iliyoletwa hapa, Serikali itatoa kwa wale ambao hawana vyeti vya kumiliki mashamba. Katika sehemu nyingi za Kenya, watu hawana vyeti vya kumiliki mashamba. Kwa mfano, kule Laikipia, kuna sehemu kama vile Thome, Marmanet na Rumuruti. Watu wanaishi bila vyeti vya kumiliki mashamba. Hati hizo zinaweza kuwasaidia kukopa---"
}