GET /api/v0.1/hansard/entries/1556251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1556251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556251/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nitoe changizo zangu kwenye statements tatu zilizoletwa na wajumbe wenzangu, nikianza na statement ya dadangu Sen. Esther Okenyuri. Ningependa kumpa heko kwa kufikiria zile jamii zinazoishi katika maisha ya kurandaranda katika miji mikuu katika taifa letu la Kenya. Sisi kama viongozi kutoka kule Pwani tumeng’ang’ana sana kuona kwamba anga ya kiwanja cha Moi kimeweza kufunguliwa ili utalii ushamiri na tuweze kupata makazi. Lakini kuna jinamizi ambalo limeibuka. Wakati watalii wanakuja katika mji wetu wa Mombasa, hizi familia ambazo hazina makaazi pale Mombasa, zinafanya vituko hadi zile juhudi zote tumeziweka kama wajumbe zinaenda na maji. Watoto hawa wanapigana mbele ya watalii na inakuwa kero kubwa. Kwa hivyo nitakubaliana na dadangu Essy Okenyuri kuwa familia hizi zitafutiwe makaazi. Pia, familia hizi zinapoendelea kutafutiwa makaazi, kuwe na viwango vya kuweza kujua ni nani ambaye anastahili kupata nyumba hizi, kumekuwa na tabia kule Mombasa, mtu anaenda kuzikwa kule bara na gari ya Matanga inaporudi, inabeba watu, baadae tunaambiwa ni familia za jamii za kurandaranda ilihali nyumbani wana mashamba makubwa, Ningependa pia kuchangia statement iliyoletwa na kakangu, Sen. Chimera, ya kwamba sisi kama serikali tunachangia mahali pakubwa kuona kwamba watu wanavamia mashamba ya wengine kwa sababu tunakawia na kuchelewesha kupeana hati miliki ya mashamba. Nitazungumzia mashamba matatu ambayo yamegawanywa ili yaweze kupewa jamii kama"
}