GET /api/v0.1/hansard/entries/1556256/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1556256,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556256/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante ndugu Spika wa Muda kwa sababu wale ndugu zangu wamekuwa wakizungumza kwa lugha ya kitaifa, ingekuwa vyema na mimi nijitahidi nihakikishe nimezungumza hivyo. Ningependa kumpa hongera dadangu, Sen. Essy Okenyuri. Jambo ambalo amelileta ni kuwa nchi yetu ikiulizwa kama kuna mpango wa kiserikali wa kujihusisha na mambo ya wale watu ambao hawana makao, ni maskini ambao wengi wao ni wazee na wale akina mama ambao wanaume wao wamefariki--- Ukiangalia watoto wengi sana kwa miji yetu ya kisasa--- Ukienda kule Kisii, uje Nairobi na kule Mombasa, utapata watoto wachanga ambao wanaishi roundabout ya Globe, wengine Uhuru Highway, na wengine wanatembea katika makaazi ya mijini, lakini sisi hatujihusishi. Kuna uwezekano wa Serikali Kuu kuwa na mpango wa affordable housing ambao serikali inajenga ili wale masikini kabisa wapewa nafasi ya kuishi? Jambo la pili, sisi kama Wabunge na wale ambao tuko hapa kama Maseneta, wengi wetu hatujazeeka. Ukienda mashinani, mababu zetu na akina mama wetu na hata wazee hawana mahali pa kuishi, hawana chakula na hawapati matibabu. Vijana na watoto wametoka na wameenda mijini mikuu. Ningependa kuuliza Bunge hili la Seneti, tujikakamue tuanze kujua vile tunaweza kuwaokoa, kwa sababu hili jambo haswa kwa serikali gatuzi ndilo tunatakiwa tujiulize kama tunaweza kutafuta njia ya kuhakikisha makaazi yamepatikana ambayo maskini wataishi. Wakati nilikuwa natafuta kura na ndugu yangu ambaye alinitoroka anaitwa Simba Arati, katika ile manifesto, tulikuwa tunasema tutajenga nyumba kule mashinani ambako maskini haswa wamama na wazee watakaa, na tuwape chakula. Hawa ni watu ambao hawana njia wala watu wa kuwahudumia, hawana madawa ama maji ya kunywa na mahali pa kuoga, Kumalizia, ningependa kusema kuwa, ndugu yangu Sen. Chimera ambaye alikuwa anazungumzia kuwa kuna mawakili wamepewa nafasi kuu zaidi ya kujiingiza kwa ufisadi. Nilikuwa katika kamati ya CPAC. Kuna kampuni za mawakili hapa nchini zinazolipwa Shilingi bilioni moja, kuwa na kesi moja ama mbili. Huu ni mpango ambao magavana wanachukua pesa za kaunti."
}