GET /api/v0.1/hansard/entries/1556258/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1556258,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556258/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa nafasi hii ili niweze kuchangia Kauli hii. Kwanza ni Kauli iliyoletwa na Mhe. Okenyuri ya kutetea wasiokuwa na makaazi. Alitaja watoto na wanawake. Lazima ifahamike wazi kwamba baadhi ya wanaume hawana makao kwa sababu wamefurushwa na wanawake watoro wasiokuwa na nidhamu. Ni lazima tunapochangia Kauli hii tutilie maanani watu wote ambao hawana makaazi. Jambo la pili ni kutaja kwa kifupi yale ambayo mheshimiwa mwenzangu alikuwa akitaja. Mheshimiwa Seneta mwenzangu alipokuwa anataja mambo ya makazi yanayoweza kugharamiwa, baadhi ya Maseneta hapa hawana makazi ya kisiasa kwa sasa. Hii ni kwa sababu walifurushwa kutoka nyumba zao za kisiasa. Sasa wanazunguka huku na kule wakitafuta makazi. Nawatakia kila la heri katika pilka pilka hizo."
}