GET /api/v0.1/hansard/entries/1556264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1556264,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556264/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Yule anayekiri kwa vitendo vyake kwamba ni mshukiwa hubwata na kujitangaza mapema kabla hajafikiwa. Tunataja mambo ya mito na ubora wa maji. Ni lazima kila kiongozi awajibike na kila taasisi iwajibike. Tumekuwa tukitaja mambo ya Mto Nairobi na watu wakiambiwa waondoke maeneo hayo. Baadhi ya viongozi walikuwa mbele wakiongoza kuzuia wananchi wasiondoke katika maeneo ya kudhibiti ubora wa mito. Hao ndio ambao Mhe. Nyutu anasema watafufua nyumba zao za kisiasa. Jambo lingine ni Kauli ya Mhe. Tabitha. Metropolitan Sacco tulijadili mambo yao katika awamu iliyopita. Sasa hivi Metropolitan wametoa notisi kwamba wanataka kubadilisha mfumo, jina na jinsi watakavyoendesha hiyo Sacco. Ni lazima tupambane na hao watu kwa sababu miongoni mwa wasimamizi wa Metropolitan Sacco ni wale walio na madeni ya zaidi ya milioni katika Sacco hiyo. Sasa sisi tuko nanyi kuhakikisha kwamba walimu na wawekezaji katika Metropolitan Sacco wanapata haki yao. Hoja ya Mhe. Chesang’ kwamba kuna baadhi ya magavana ambao kazi yao ni kuzurura na kutoa cheche za matusi na kejeli kwa Serikali. Lazima mikoba ya Serikali na pesa zetu tuzilinde kwa sababu hawa magavana hawana msingi madhubuti wa kutosomea sisi viongozi jinsi tunavyopaswa kufanya kazi. Hizo pesa ambazo wanatumia kwenda kwa vyombo vya habari---"
}