GET /api/v0.1/hansard/entries/1556388/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1556388,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556388/?format=api",
    "text_counter": 46,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "zitafika katika Kenya nzima, haswa sehemu zetu za gatuzi ambazo ziko kando kando? Kwa mfano, katika sehemu yetu ya Tana River, utakuta kwamba simu za rununu zinafanya kazi katika miji mikubwa pekee yake. Ukiingia ndani, unapata shida ya mawasiliano. Je, kuna mpangilio maalum katika Wizara ambapo pesa zimetengwa ya kusema kwamba mwaka huu, pesa fulani zitatumika katika area fulani huko Tana River, ili kuweka mtandao wa simu na mwaka ujao itakuwa gatuzi lingine? Kama huo mpango upo, tafadhali table huo mpango hapa ili tujue huo mpangilio na pesa ambazo Serikali imeweka kwa ajili yake. Tusiwe tu tunakuja hapa kuuliza maswali; tunafaa tuwe na mpangilio sawa sawa. Asante, Bw. Spika."
}