GET /api/v0.1/hansard/entries/1556853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1556853,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1556853/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nimuunge mkono Mbunge mwenzangu. Imebainika wazi kuwa wanaendesha magari mbio sana na kusababisha ajali. Hata Mombasa, mtu atakwambia, “mbona unaenda mbio kama gari la miraa?” Hii ni kumaanisha kwamba jambo hili linajulikana, na ni gari zote za miraa. Juzi kuna Mheshimiwa alikuja hapa kusema kuwa Meru kuna ugonjwa wa saratani sana. Nataka kurejelea na kusema kuwa hizi gari zinazopeleka mmea huu mbio, ndizo zinazisindikiza ugonjwa wa saratani sehemu zingine. Kwa yote, nasema kuwa zinaenda kwa kasi sana. Nampongeza Mheshimiwa mwenzangu kwa kupendekeza waweze kupunguza ile kasi ambayo wanaziendesha gari zile. Sijui hukimbia kwenda wapi."
}