GET /api/v0.1/hansard/entries/1557044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1557044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557044/?format=api",
    "text_counter": 473,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Carren alionyesha weledi wa kuweza kuangalia masuala ya watoto. Kama tunavyofahamu katika taifa hili, masuala ya watoto yameachwa kando na hayajazingatiwa vizuri. Kwa hivyo, tulimpiga msasa kwa kuuliza maswali, na aliweza kuyajibu kwa uweledi. Nina imani kuwa wale maofisa watakaofanya kazi chini yake, pamoja na elimu yake, watamuwezesha kufanya juhudi zaidi ili kusaidia watoto. Ni msomi, mjasiri na nampongeza kwa kuteuliwa katika Idara hii."
}