GET /api/v0.1/hansard/entries/1557050/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1557050,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557050/?format=api",
    "text_counter": 479,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "waliokuja na kuwapa mbinu za kuwekeza. Kwa sasa, SACCO hiyo ya Kilifi imebobea katika sekta ya bodaboda Kenya nzima kwa sababu ya akili ya kijana mdogo, Fikirini Jacobs. Yale maneno aliyokuwa anazungumza na Chairman wangu aweze kukubali, tulikuwa na raha mpaka tulikuwa twaonelea kumwambia kuwa awache maswali mengine, isipokuwa ni ule mwelekeo ambao tulikuwa nao kuwa lazima tuyamalize maswali yote. Nampongeza sana Bw. Fikirini Jacobs. Nakuombea Mungu akuelekeze katika kazi hii ili uinue vijana wa Kenya. Na si yeye pekee yake, niliona pia yule Bw Makokha, ambaye amepewa State Department for Economic Planning, The National Treasury and EconomicPlanning amesoma na kubobea. Amesema kuwa atahakikisha kuwa ataweka sheria ambazo zitahakikisha madeni ambayo Kenya imekopa yanalipwa kwa wepesi. Nikimalizia, nachukuwa fursa hii kumshukuru Rais wa taifa hili, Dr William Samoei Ruto, kwa kutoa mwanya wa Broad-Based Government ili waweze kuleta akili ambazo zimebobea na zinazoweza kuendeleza hili taifa mbele. Nampongeza sana kwa kuchukua kijana wetu wa Kigiriama. Tulikuwa tumeachwa nyuma, lakini mara hii, Mama Zamzam ninatabasamu na kusema Bw. Fikirini atainua Wagiriama, Pwani na vile vile Kenya nzima. Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Nawatakia kila la heri."
}