GET /api/v0.1/hansard/entries/1557059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1557059,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557059/?format=api",
"text_counter": 488,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, ODM",
"speaker_title": "Hon. Irene Mayaka",
"speaker": null,
"content": "kuwa kijana yeyote anaweza kupata kazi kubwa kama hii. Bw. Fikirini ametoka huko Kilifi, na hakuna mtu ambaye angedhani yakuwa aliweza kuhitimu vile, lakini yeye mwenyewe alijieleza kinaga ubaga. Wenzangu na Wakenya wote tumeona kweli kabisa kuwa Serikali ya msingi mpana inaunga mkono sana watu ambao wamehitimu kufanya kazi. Mhe. Spika wa Muda, namshukuru sana Baba Raila Amolo Odinga kwa kutupa wateule ambao wamehitimu, kama Bw Fikirini, Bi. CPA Carren, Daktari Makokha, Bw Cyrell na Mhe. Ahmed. Wote wameonyesha kwamba wamehitimu na ni watachapa kazi. Nachukua fursa hii kumshukuru Rais wa nchi hii kwa sababu ameona ni vizuri tuwe na watu ambao wametoka katika maeneo mbalimbali ya nchi hii, ambao wanaweza kutumikia Serikali katika hali ya juu. Kwa hayo mafupi, naomba Jumba hili liwapitishe hawa vijana. Pia, nawahimiza wenzangu tukiwa huko nje, lazima tuzidi kuwaambia watu wapatie Serikali fursa ya kufanya kazi katika nchi hii. Watu ambao wamehitimu watumikie nchi hii, ili tuonyeshe kweli Serikali ya msingi mpana inaweza kufanya kazi nzuri. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii maalum. Asante sana."
}