GET /api/v0.1/hansard/entries/1557062/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1557062,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557062/?format=api",
"text_counter": 491,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Nachukua fursa hii nikushukuru kwa kunipa nafasi hii. Pia, nashukuru Kamati ambayo imeongoza kukaguliwa kwa hawa wawili chini ya uongozi wa Mwenyekiti, Mhe. Alice Ng’ang’a. Namshukuru zaidi kwa sababu ya kuweza kunakili kwa utaratibu na uzoefu, na kueleza vizuri kuhusu hawa wateule wawili. Kutoka Kilifi, nataka kuzungumzia kuhusu kijana Fikirini Jacobs Katoi Kahindi, anayetoka kule Ganze, ambapo ni reserve ya Kilifi kabisa. Ukitajiwa Ganze ndani ya Kenya hii, unafikiri ni mahali hakuna maji wala chakula. Wakipata chakula, huwa tunakiita ni cha msolo. Chakula cha msaada kinapelekwa kule. Hapa tumepata kijana Fikirini Jacobs, ambaye amesoma kwa bidii na michango. Anaongoza vijana na ana sauti kubwa ndani ya Kilifi. Kwa uweledi wa kupenda masomo, kijana huyu amehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Pwani, ambao ni mwelekeo mzuri. Vijana wengi hutaka waje Nairobi wapate shahada zao. Lakini huyu alianza huko bara, na mwisho amepata shahada katika Chuo Kikuu cha Pwani. Nawapongeza wahadhiri wote wa Chuo Kikuu cha Pwani kwa kumshikilia huyu kijana mkakamavu."
}