GET /api/v0.1/hansard/entries/1557074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1557074,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1557074/?format=api",
    "text_counter": 503,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Nilikuwa nazungumzia kuhusu kijana Fikirini Jacobs Katoi Kahindi kutoka Ganze, Kilifi. Namshukuru Mhe. Rais William Samoei Ruto kwa kumteua katika Wizara ya Maswala ya Vijana na Uchumi Bunifu. Katika nguvu zake na umri wake wa miaka thelathini, kijana huyu ni kielelezo kizuri sana kwa vijana wenzake wanaotafuta kazi. Kwa hivyo, namshukuru Rais kwa kumteua kijana kutoka Kilifi ambaye atawapa vijana wa Kilifi mwelekeo. Mihadarati inawaathiri vijana Kenya nzima, haswa pale Kilifi. Fikirini ni kijana aliye na mvuto mzuri kwa vijana wenzake. Najua akiwaita vijana katika mkutano awazungumzie kuhusu mihadarati kule Pwani na Kenya nzima, vijana watafuatiliza maelezo yake. Kijana huyu amekuwa mzuri sana katika Ofisi ya Gavana wa Kilifi, Mhe. Gideon Maitha Mun’garo, akiwa katika kitengo cha utoaji wa huduma. Ni kijana mwenye maarifa. Angetoa taarifa katika mikutano bila kuangalia karatasi na kuangazia kazi zote za Mhe. Gavana Mun’garo. Kwa hivyo, namshukuru Rais na Kamati hii inayoongozwa na dadangu, Alice Ng’ang’a, kwa kumpitisha kijana huyu. Tunajua atakuwa muhimu sana katika kuzingatia masuala ya vijana na uchumi bunifu Kenya nzima. Tunamshukuru Rais kama watu wa Kilifi. Nimeipinga sana Serikali hii, lakini katika jambo hili, namshukuru Mhe. Rais, kwa niaba ya viongozi wa Kilifi katika Bunge hili. Amchukue kijana huyu atakayefanya kazi Kenya nzima. Namshukuru babangu, Raila Amolo Odinga, kwa kukubali kijana huyu ateuliwe. Ni kijana wake mwenye sauti kubwa sana, ambaye angesimama katika mkutano kumtetea Raila. Lakini Raila amemruhusu afanye kazi ya Serikali. Sisi kama viongozi wa Kilifi tunalikubali jambo hilo. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}